Dkt Stergomena Tax
Dkt Stergomena Tax
Wasifu
Dkt. Stergomena Lawrence Tax ni mwanadiplomasia, na mtaalam wa masuala ya utangamano wa kikanda, (regional integration). Ana uzoefu wa zaidi ya miongo mitatu ya uongozi wa juu katika masuala ya utawala, amani na usalama, mchakato wa kidemokrasia, diplomasia, na sera na mikakati ya kiuchumi. Uteuzi wake kuwa Mwanachama wa Tume ya Uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa October, 2025 nchini Tanzania unaakisi historia yake ya uadilifu, weledi, na utaalamu katika kuzuia migogoro, upatanishi, na uimarishaji wa taasisi