TUME Logo
TUME Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025
Mwenyekiti wa Tume
Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman Mwenyekiti wa Tume
Karibu

Karibu kwenye Tovuti ya Tume ya Kuchunguza Matukio yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. 

Huu ni Ukurasa Maalum wa kutoa maoni, uzoefu na mapendekezo ili kuiwezesha Tume kufanya uchunguzi wa kina, wa haki, na jumuishi, na hatimaye kubaini chanzo cha matukio haya, kutathmini hatua zilizochukuliwa, na kuainisha mapendekezo ya hatua stahiki za kurejesha na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa. Kwa heshima kubwa, tunawakaribisha wadau wote, wakiwemo Wananchi, Asasi za Kiraia, Taasisi za Serikali, Taasisi za Kidini, Viongozi wa Jamii, Vyama vya Kitaaluma, na makundi mengine kushiriki.

Tume inathamini maoni yote yatakayopokelewa kwani yatakuwa ni msingi wa kujenga maridhiano ya Kitaifa.

Karibuni sana 

Angalizo
Tume inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria. Kwa hiyo, tunawaomba wadau wote kutoa taarifa, ushahidi, maoni, na mapendekezo yenye usahihi, uadilifu na ukweli, ili kuisaidia Tume kufanya Uchunguzi wa Kina na Kutoa mapendekezo yenye tija kwa Taifa.
Wasiliana Nasi