Balozi David Joseph Kapya
Wasifu
Balozi David Joseph Kapya, ni Balozi na mwanadiplomasia mwandamizi ambaye amewahi kuwa msaidizi mahususi wa Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Willium Mkapa katika mazungumzo ya kutatua migogoro na kuleta amani mashariki ya DRC, amekuwa msaidizi mahususi wa Rais wa awamu ya tatu katika usuluhishi wa mgogoro wa Sudan, juhudi ambazo zilipelekea kuzaliwa kwa taifa jipya la Sudan Kusini. Amekuwa mshauri mahususi wa Rais wa awamu ya tatu katika upatanishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, awahi kuwa mdaidizi mahususi wa rais wa awamu ya nne Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika timu ya Umoja wa Afrika ya Usuluhishi wa Mgogoro Nchini Ivory Coast, na amewahi kuwa mwakilishi maalum wa Tanzania kwenye utatuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini Zimbambwe.