Said Ally Mwema
Said Ally Mwema
Wasifu
Said Ally Mwema ni Mkuu wa jeshi la Polisi mstaafu, ambaye amewahi kusimamia maboresho makubwa ya Jeshi la Polisi ikiwemo kuandaa mkakati na utekelezaji wa Polisi Jamii. Akiwa Mkuu wa Jeshi la Polisi pia aliongoza Jeshi kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo uhalifu wa kuvuka mipaka, ugaidi, biashara haramu ya binadamu na madawa ya kulevya. Amewahi pia kuwa Mkuu wa Kanda ndogo (sub-region bureau) ya Interpol iliyopo Nairobi Kenya, na alikuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya kuangalia jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai.