TUME Logo
TUME Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025

Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman

Mohamed Chande Othman photo
Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman
Mwenyekiti wa Tume

Barua pepe: mohamed.othman@tume.uchunguzi.go.tz

Simu: 0743040890

Wasifu

Mheshimiwa Jaji Mohamed Chande Othman ana uzoefu na weledi mkubwa katika masuala ya sheria, haki za binadamu na utunzaji wa amani. Amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 2010 hadi 2017, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Amewahi kushiriki kama mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa katika Uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Lebanon na Sudan. Amewahi kuwa Mjumbe wa Timu ya Kupitia Sheria iliyoanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Amewahi pia kuwa mjumbe wa Timu huru ya wataalamu ya kutathmini utendaji na ufanisi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, amewahi kuwa mwendesha mashtaka mkuu katika kesi za uhalifu uliotokea nchini Timol Mashariki, amewahi kuwa mwendesha mashtaka katika mahakama ya umoja wa mataifa ya uhalifu wa mauaji wa Rwanda, Pia alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini

Wasiliana Nasi